20 Mar, 2018

KUANZIA DHANA YA KUSISIMUA HADI KUFAULU

Mahojiano yaliyofanywa na Mkuu wa zamani wa BBC Africa Peter Burdin na mwanzilishi wa ESSA Patrick Dunne

Je, nini kilikuwa cheche kwa wazo la ESSA?

Wazo la ESSA lilizaliwa katika shule za vijini vya Afrika kutokana na kusikiliza wanafunzi, waelimishaji, watunga sera na watoa misaada kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Ilikuwa ni mchanganyiko wa kuona fursa kubwa ya kusaidia kufanya mambo kuwa bora na kuchochewa zaidi na mhangaiko

Daima ni vyema kujitahidi wakati kitu kinaendelea vizuri. Njia yangu ni "Fikiria nini ungeweza sasa?" nyuma yake na hivyo ndivyo ESSA iliibuka. Ilionekana tu kama jambo la kawaida baada ya kuona na kujifunza mengi kutoka kwa Warwick barani Afrika.

Tulikuwa tumeanzisha Warwick barani Afrika mwaka 2006 na tunawafundisha wanafunzi na kuwafundisha walimu katika makazi duni na katika maeneo ya mashambani yaliyo na umaskini mkubwa nchini Ghana, Afrika Kusini na Tanzania. Kufikia mwaka 2015, shirika letu changa la £30,000 lilikuwa limewanufaisha zaidi ya vijana 250,000 Waafrika na zaidi ya walimu 2,000 (ni zaidi ya wanafunzi 465,000 na walimu 3,000 sasa). Tulikuwa tunakuwa kwa kasi, na kufanikisha athari kubwa na 'athari zetu kubwa kwa kila shilingi' zilikuwa zinaonekana. Hata hivyo, kwa uhalisia tulikuwa shirika dogo ikilinganishwa na ukubwa wa tatizo. 

Pia kulikuwa na vitu vingine vingi sana kando na mafundisho na mafunzo ya moja kwa moja ambayo yalihitajika ili kubadilisha matokeo ya kielimu. Nilikutana na watu wengi ambao walijua kile kilichohitajika lakini kwa kusikitisha hawakuwa na fursa ya kupata au kuhamasisha rasilimali zinazohitajika ili kufanya mabadiliko ambayo walitaka kuona. Wakati huo huo makampuni na wakfu zilikuwa zikilalamika kuhusu ukosefu wa miradi inayoweza kuungwa mkono na watu kuifanya. Ilionekana kuwa sekta ambayo haikuwa ambapo kuna mashirika mengi na watu wanaofanya mambo na kupata mafanikio kwa viwango tofauti-tofauti. Yote bila kufikia malengo hitajika.. 

Ni lazima kungekuwa na njia bora zaidi na ikiwa kungekuwa na uwezekano wa kuunda kitu ambacho kingeweza kuunganisha, kufahamisha, kuhamasisha, kuzingatia na kuongeza athari kwa kila mtu anayewekeza katika elimu Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, basi inaweza kuwasaidia watu kubadilisha matokeo ya kielimu

Patrick Dunne

Patrick Dunne, Founder

Je, ni kweli kwamba dhana ya kwanza ya ESSA ilitolewa kwenye mfuko wa wagonjwa kwenye ndege kutoka mjini Accra hadi Johannesburg?

Ndio kabisa! Usafiri, hasa barani Afrika ni wa kusisimua. Hakukuwa na nafasi ya kulala, betri ya kipakatilishi changu ilikuwa imekwisha na nilikuwa nimemaliza makaratasi. Mfuko wa wagonjwa ndio pekee ungeweza kurekodi kile kilichofikiria.

Kama mtaalamu wa hisabati nilifadhaishwa na ukosefu wa takwimu za ubora wa juu kuhusu elimu barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara pamoja na masuala kadhaa ya kimfumo kama vile "Walimu hewa" ambalo lilionekana kuwakaidi. Pia hapakuwa na mahali moja ambapo unaweza kwenda mtandaoni ili ujue mambo yote unayohitaji kujua kuhusu elimu katika kandan hii. Kwa mfano, ni nani mwingine anayefanya kile tunachotaka kufanya, ni utafiti upi bora kuhusu unachohitaji kujua, watafiti wakuu ni nani, ni nani anaweza kuwa mshirika mzuri, ni mifano gani ya athari kubwa zani, ni nani anayefadhili nini na ni takwimu zipi na mahitaji yapi muhimu ya kanda au mada au mengine . Warwick barani Afrika ilikuwa imenufaika na mikutano mingi ya  kile kinachoita 'wahamasishaji wakuu' katika sekta hii lakini hapakuwa na mtandao wazi au jukwaa la kubadilishana mawazo au kujifunza kutoka kwa wengine katika sehemu mbalimbali za sekta hii.

Kwenye mfuko wa wagonjwa niliandika mambo manne ambayo biashara mpya ya kijamii inaweza kufanya ili kusaidia. Haya yalikuwa:

  • Kujiunga"

  • "Kituo cha Maarifa cha Kutegemewa"

  • "Kujua mambo ambayo watu wanataka na wanahitaji sana kujua"

  • "Ujengaji uwezo"

Jinsi ambavyo unafanya mambo ni muhimu kama mambo unayofanya hivyo basi nikaandika maneno machache kuhusu jinsi ambavyo tunaweza kufanya mambo.

  • "Maeneo mbalimbali" ina maana watu wanafanya mambo kote Afrika na kwingineko badala ya yote katika ofisi moja kuu.

  • "Inaongozwa na Waafrika" ina maana bodi na timu zina Waafrika wengi na zina Mwenyekiti na Afisa Mkuu Mtendaji Mwaafrikana nao vijana Waafrika wakihusika zaidi.

  • "Ushirikiano" Kazi nyingi nzuri zimefanyika na watu wengi kwa muda mrefu ambao walijua mengi zaidi kuliko mimi. Ilikuwa ni muhimu kuwashirikisha, kujifunza kutoka kwao na ikiwezekana kufanya chochote tungeweza ili kuwasaidia kufanikisha athari kubwa zaidi.

  • Imani yangu ya "Athari kubwa kwa kila shilingi". Kuchangisha fedha ni vigumu, muda ni mfupi na haja ni kubwa kwa hivyo kupata athari kubwa zaidi kwa kila shilingi ni muhimu.

Watu wengi wameniuliza kwa nini hatukuongeza shughuli za ESSA kwenye Warwick barani Afrika kulingana na sifa zake. Rahisi, "Malengo". Warwick barani Afrika kuzingatia utoaji wa moja kwa moja kumekuwa muhimu kwa mafanikio. ESSA inafanya kitu tofauti kabisa. Uzingatiaji utaendelea kuwa mkali jinsi tunavyolenga kujenga hatua kwa hatua. Kila hatua pia itahitaji lengo kubwa ili kufanikiwa na kuwa na kundi lake la metriki za athari.

Ni vyema kwamba vipimo vinne muhimu vya ESSA vimesalia thabiti na vinaanza kuwa uhalisia. Maoni ya mapema kutoka kwa wale tunaofanya kazi nao yanaonyesha kwamba tunaendesha mambo kulingana na jinsi tunavyotaka kufanya mambo. 


Kwa hiyo, dhana ya ESSA ilitokaje kwenye mfuko wa wagonjwa na kuwa kitu ambacho unaweza kupata uungwaji mkono mkubwa?

Kama ilivyo kawaida iloitegemea kuwa na marafiki wa ajabu ambao walishiriki maono haya, waliifanya tofauti na kusaidia kuifanya kuwa kitu ambacho hatimaye kilipata ufadhili na msaada mwingine kutoka kwa Wakfu kuu barani Ulaya, Wakfu wa Bosch.

Mmoja ya wakarimu hawa alikuwa Mary McGrath mkurugenzi wa maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick ambaye alikuwa mwanzilishi mwenzo wa Warwick barani Afrika. Mary alikuwa alikuwa amekumbana na tatizo hili moja kwa moja na pia alilielewa kwa mtazamo wa taasisi kuu ya elimu kama vile Warwick. Kisha, baadhi ya wasomi katika Warwick wakachangia dhana hii kwa kuichambua na kufauru jaribio.

Phumi Mthiyne, mwalimu kutoka makazi duni ya Alexandre, Johannesburg ni mtu mwingine ambaye alichangia pakubwa. Mafanikio yake katika Shule ya Upili ya Realogile yamekuwa ya ajabu. Si tu kwa sababu ya matokeo ya moja kwa moja na mkondo thabiti wa vijana kutoka huko, hasa wasichana, kuingia katika Vyuo Vikuu bora nchini Afrika Kusini. Yeye na wenzake pia walikuwa wameonyesha kwamba uwekezaji mdogo kwa walimu wenye ujuzi na ubunifu unaweza kuwa na athari kubwa. Kuwekeza katika masuala ya watu kwa njia sawia ikiwa si zaidi kwa vitu vinavyoonekana.

Chris Foy, mwanachama wa zamani wa Baraza la Chuo Kikuu cha Warwick akawa mwanzilishi mwenza. Chris alizaliwa barani Afrika na alitumia muda mwingi maishani mwake kujenga biashara mbalimbali kote barani Afrika. Kisha pamoja tulifanya kazi na Mwanafunzi wa PhD Mnaijeria kutoka Warwick, Tosin Ige, ambaye alifanya utafiti sahihi kuona kama kulikuwa na haja halisi na kama mtu yeyote amefanya kile tulijaribu kufanya. Kwa mara nyingine tukapita katika lango huo.

Kulikuwa na njia mbili za wazi ambazo tunaweza kufuata kimpangilio. Ya kwanza, kutokana na shauku kati ya wasomi mbalimbali wa Warwick, ilikuwa kujenga kituo kipya cha Afrika katika Warwick. Njia ile nyingine ilikuwa kujenga kipengele kipya huru. Uchaguzi ukawa rahisi tulipokuwa tukifikiri juu ya jinsi ya kufanya ESSA kuongozwa na Waafrika ifaavyo na hivyo ndivyo tulitaka iwe.

ESSA haingeweza kuwa inaongozwa na Waafrika kikamilifu, licha ya kuongozwa na Waafrika ikiwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Uingereza. Aidha, wakati huo haukuwa mwafaka kwa Warwick katika tukio lolote kwani Warwick ilikuwa karibu kufanya uwekezaji mkubwa kwingineko uliotumia ambao ulikuwa unatumia rasimali za usimamizi na maendeleo.

Baada ya uamuzi huu wa mwanzo mpya kabisa kufanywa, hatua iliyofuata ilikuwa kuweka mambo samabamba na kupata ufadhili mzuri, na wafadhili waliokuwa na sifa katika sekta hii. Ni wakati huu Septemba 2015 tulibahatika kweli.

Rafiki mzuri na muungaji mkuu wa Warwick barani Afrika, mtangazaji wa BBC Kirsty Lang pamoja nami tulikuwa tunakula chakula cha mchana. Kirsty ameishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini. Nilipomwambia kuwa sasa tuko tayari kujaribu kuchangisha fedha nyingi kwa ajili ya ESSA mara moja alisema kwamba tunapaswa kuzungumza na Wakfu wa Bosch ambao alikuwa ameongoza kongamano lao hivi majuzi mjini Berlin.

Wiki kadhaa baadaye nikakutana na Olaf Hahn kutoka Wakfu wa Bosch na kisha baada ya miezi michache tu, baada ya mazungumzo thabiti, tulipata ahadi ya kwanza ya £ milioni 1 pamoja na msaada wa aina nyingi ikiwa ni pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji wa Wakfu wa Bosch Uta-Micaela Dürig kujiunga na Bodi.


Jina ESSA linatoka wapi?

Kupitia kazi yangu ya kemikali, kampuni binafsi na za kijamii nimekuwa na bahati kubwa ya kukutana na watu wengi wenye shauku nyingi. Wawili yao, Carrie Stokes na Gill Thomas, ni wataalam wa bidhaa na wamefanya kazi ya ajabu katika kusaidia 3i na Leap Confronting Conflict katika ukuzaji bidhaa yao. Ni haraka sana kuwageukia Carrie na Gill kwa ajili ya mambo kama hayo na wakafurahishwa na wazo la ESSA na wakasaidia bila malipo.

Kama kawaida maswali yao, tafiti  za kina na mawazo yao yalipelekea kubuni jina hili. Swali lao rahisi lilikuwa "Je, unataka jina ambalo lenyewe linalosema kile mnachofanya au unataka jina jipya ambalo utawekeza ndani yake ili lilinganishwe na kile mnachofanya?". Hatukutaka kutumia wakati au pesa katika kujenga jina jipya. Jina letu la kufanya kazi lilikuwa "ESSA-Education Afrika Kusini mwa  Sahara" (Elimu barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara). Kwa hiyo, tulijaribu ESSA kwa watu mbalimbali na likakubalika vizuri.


Je, inaendaje, mwaka mmoja baada ya kuanza?

Kama unavyoona kwenye tovuti yetu, hadi sasa inakwenda nzuri sana. Hili ni shirika langu la nne la kijamii na kama tunavyojua kuanzisha shirika jipya kuna changamoto chungu nzima. Kwa hiyo, imekuwa ni changamoto nyingi!

Tuliweza kusajiliwa kisheria kwa haraka kwa ushauri mzuri kutoka kwa kampuni ya sheria ya London ya Bates Wells Braithwaite na umakinikaji wa Chris katika maelezo ya kina. Sisi pia tulibahatika kuwa na mfadhili wetu mkuu wa kwanza Wakfu wa Bosch ambaye amekuwa mshirika wa ajabu na ameongeza thamani nyingi kwa njia nyingi sana kupitia Olaf na Uta-Micaela. Pia waliitikia vizuri ombi langu la kipekee kwamba Olaf aungwe mkono kuwa Mkurugenzi Mwanzilishi wetu wa ESSA wakati inapoanza na kisha kumwajiri mrithi wake Mwaafrika. Usimamizi wa mradi wa Olaf, ujuzi wake wa uhusiano na lugha pamoja na mtandao wake umetuwezesha kuendesha mambo kwa ufanisi.

Pia tumeweza kuweka Waafrika katika kitovu cha kila kitu tunachofanya, sio tu kwa ushirikiano ulio hapa juu lakini pia kwa njia nyingine nyingi. Wanafunzi Waafrika waliusaidia Wakfu wa Bosch kufanya bidii yao, walimu na wanafunzi Waafrika katika shule za Warwick barani Afrika na kwingineko wamehusika katika warsha nyingi za kutoa mchango na changamoto, na wanafunzi Waafrika watafanyia kazi miradi yetu yote 12 ya sasa. Lengo letu ni kuwa na Bodi yenye Waafrika wengi punde iwezekanavyo, na tumeanza vizuri kwa kumteua Joel Kibazo, mkuu wa biashara ya Afrika ya FTI na mkurugenzi wa zamani wa mawasiliano kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Joel ataungana hivi karibuni na mfanyabiashara mashuhuri Mwaafrika katika jumuiya ya utoaji msaada.Kwa kuzingatia mkabala wetu wa hatua kwa hatua, tuliamua kuweka msisitizo wa mapema kwenye Elimu ya Juu. Kwa nini? Vizuri kwa kuwa taasisi za Elimu za Juu ni vituo vya kielimu vya kanda katika maeneo mengi barani Afrika na pia kuwa waendeshaji ukuaji wa kiuchumi na kijamii. Pia zinawafundisha walimu, zinafanya utafiti kuhusu elimu katika nchi zao, zinashawishi utungaji sera na zina uhusiano mzuri na waajiri nchini na serikali za mitaa. Kando na hayo, pia zinaongoza katika sekta ya elimu na tukahisi kwamba kama tunaweza kufanya mambo ambayo yatazisaidia basi tunaweza kujenga juu ya hayo.

Hii inaonekana kuwa na matokeo mazuri kama unavyoona kutokana na ushirikiano ambao tumeanzisha na kazi tunayofanya


Nini kinachofuata?

Tumekuwa na mwanzo mzuri lakini kuna mengi zaidi ya kufanya. Mtazamo wetu kwa sasa ni: kuwasilisha athari kubwa kutokana na miradi na kazi inayoendelea, kuchangisha ufadhili muhimu wa ziada wa miradi, kukuza na kuongeza ushirikiano wetu, kuendelea kujenga Bodi na timu yetu na kuwekeza katika kujenga uwezo wetu wa dijitali, jumuiya za mitandao ya kijamii na shughuli za kituo cha maarifa.

Juu ya hayo, kwa sababu tunafanya safari nyingi za ndege, nina matumaini kutakuwa na nyakati nyingi za dhana za kusisimua!

Comments

About text formats

Restricted HTML

  • Allowed HTML tags: <a href hreflang> <em> <strong> <cite> <blockquote cite> <code> <ul type> <ol start type> <li> <dl> <dt> <dd> <h2 id> <h3 id> <h4 id> <h5 id> <h6 id>
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.